Lydia Mollel – Morogoro.

Mtangazaji wa Zamani wa Shirika la Habari la Uingereza – BBC, Salim Kikeke amewataka Vijana Nchini kuwa na ndoto zenye malengo, ili waweze kupata mafanikio kwenye maisha yao.

Kikeke ameyasema hayo Mkoani Morogoro katika kongamano lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Ufaulu Project kupitia kampeni maalum ya Nje ya boksi, lililowakutanisha Vijana zaidi ya 1,500 wa Vyuo mbalimbali Mkoani hapo, ili kuwajengea uwezo wa kifikra pamoja na fursa za ajira.

Amesema, “kama umefika mahali na ukasema unataka kuwa University drop-out plan A yako ndio plan B yako yaani plan A ikifeli ile plan B yako ndio plan A.”

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Alaudin Hasham amewataka vijana kujua kile wanachokihitaji kwani ndio mwongozo wa yeye kuweza kupata mafanikio kwani akuna aliyezaliwa kufeli.

“Kama ujafeli maana yake ujajaribu na kama unataka kumiliki ambacho huna nilazima ufanye kitu ambacho ujawai kukifanya tusiwe watu wa kukubali kushindwa kwa haraka,” alisema Alaudin.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ufaulu Project Simon Chami amesema wanashirikiana vyema na wadau katika kuhakikisha Vijana wanajifunza mambo mbalimbali, ikwemo elimu ya fedha, kufunguka kifikra na kujua namna ya kutengeneza fursa za kujiajiri, ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Paul Pogba kuigiza 4 Zeros
Balozi Kombo: Kiswahili ni fursa kitumiwe kukuza uchumi