Mshindi wa Kombe la Dunia, Paul Pogba, ataigiza katika filamu ya Ufaransa itakayotolewa Aprili 2025 baada ya kurekodi matukio ya video mjini Paris wiki hii, vyanzo vimeiambia ESPN.

Pogba anatumikia kifungo cha miaka minne kwa ukiukaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli ambayo ilitolewa Februari mwaka huu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Kimataifa wa Ufaransa, alisema wakati huo kuwa hajawahi kuchukua kwa makusudi dawa zilizopigwa marufuku na alipanga kukata rufani dhidi ya uamuzi huo.

Filamu hiyo inaitwa 4 Zeros, na ni mwendelezo wa 3 Zeros iliyotolewa mwaka 2002.

Kwa mujibu wa Jarida la Ufaransa la Le Parisien, ambalo liliripoti kwa mara ya kwanza kuhusu nafasi ya Pogba katika filamu hiyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, atacheza kama kocha wa timu ya vijana.

Rufani ya Pogba kuhusu shtaka hilo la matumizi ya dawa za kusisimua misuli litasikilizwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ‘CAS’, na iwapo rufaa yake itafanikiwa, adhabu yake inaweza kupunguzwa.

Ten Hag amtolea uvivu Jose Mourinho
Kikeke: Vijana pambanieni ndoto zenye malengo