Kocha Mkuu wa Manchester United Erik ten Hag amejibu maoni yaliyotolewa na Jose Mourinho baada ya kocha huyo kutoka nchini Ureno kusema kuwa hakuwahi kuwa na uungwaji mkono kama Mholanzi huyo pale Manchester United.

Mourinho alipendekeza kuwa Ten Hag amepewa uungwaji mkono zaidi katika usajili wa wachezaji kuliko ilivyokuwa wakati wa ukufunzi wake klabuni hapo uliodumu kwa miaka miwili na nusu.

Hata hivyo, Ten Hag amejibu kwa kudai kuwa Mourinho ndiye kocha pekee katika zama za baada ya Sir Alex Ferguson kupata wachezaji anaowataka.

“Mbali na Mourinho, kocha mwingine hakupata wachezaji aliotaka, na hicho ndicho unachohitaji,” alisema Ten Hag katika mahojiano na ESPN Brasil.

“Nina imani tutafikia malengo yetu, lakini ni mashindano magumu, si mbio za farasi wawili tena.

“Kuna saba, nane (timu kwenye Ligi Kuu) ambazo zote zinakwenda kwa ajili ya ubingwa, ambazo zote zina vikosi vizuri sana. Hivyo kama unataka kutwaa ubingwa, lazima utengeneze kikosi hicho.”

Ten Hag anakabiliwa na mustakabali usio na uhakika ndani ya United baada ya kuwa na msimu wa pili usioridhisha.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 54, amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, lakini hajapewa hakikisho rasmi na mmiliki mwenza mpya Sir Jim Ratcliffe kama ataendelea kuwa kocha zaidi ya msimu wa majira ya joto.

Kocha huyo wa zamani wa Ajax alijaribu bila mfanikio kuwasajili wachezaji kama Frenkie de Jong na Harry Kane, lakini akasema uamuzi wa klabu hiyo kuleta wachezaji wachanga kama Rasmus Højlund unamaanisha kwamba anapaswa kupewa uvumilivu ili kurekebisha mambo.

“Unahitají wachezaji bora. La sivyo, uko kwenye mchakato na lazima uwe na subira. Hapo ndipo tulipo.” alisema Ten Hag.

Mawakala usafirishaji Wahamiaji haramu waonywa
Paul Pogba kuigiza 4 Zeros