Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji FC, Kassim Lyogope amesema timu yake itajipanga vizuri ili kupata ushindi katika michezo yao sita ya Ligi Kuu iliyobakia ili iweze kubakia katika Ligi Kuu.

Lyogope amesema hayo jana wakati wa mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Amesema pamoja na kupoteza dhidi ya Singida Fountain Gate, bado hawajakata tamaa na wataendelea kupambana ili kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Malengo yetu yapo palepale kuhakikisha tunabakia katika Ligi Kuu. Bado michezo sita ligi iishe ila nina imani timu yangu itafanya vyema kutokana na ubora wa timu yetu,” amesema

Amesema timu yake itarejea jijini Dodoma kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa ljumaa (Mei 11) katika Uwanja wa Jamhuri.

Amesema Mei 13 timu yao itacheza dhidi ya Namungo FC, Mei 16 itacheza na Simba SC.

Ameongeza kuwa Mei 22 watacheza dhidi ya Young Africans. Michezo yote hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Dodoma Jiji ipo katika nafasi ya 10 ikiwa na alama 23 baada ya michezo 24 iliyocheza.

Beki wa Dodoma Jiji FC, Ngalema Abubakary amesema pamoja na wenzake, wataendelea kupambana ili kusaidia timu yao iendelee kuwepo Ligi Kuu Bara msimu ujao 2024/25.

Balozi Kombo: Kiswahili ni fursa kitumiwe kukuza uchumi
BURUDANI: Kifo kilitenganisha 'bifu' la Papa Wemba, Koffi Olomide