Klabu ya Chelsea imefanya mawasiliano na SSC Napoli kuhusu uwezekano wa kubadilishana mkataba unaowahusisha washambuliaji Victor Osimhen na Romelu Lukaku, ripoti imedai.

Kumpata Mshambuliaji mpya kwa muda mrefu kimekuwa kipaumbele cha kwanza kwa Chelsea katika dirisha la usajili la majira ya joto, huku Osimhen akionekana kama mgombea anayeongoza kwa sehemu kubwa ya msimu.

Mnigeria huyo alisaini mkataba mpya na SSC Napoli mapema mwaka huu ambao una kipengele cha kutolewa chenye thamani ya zaidi ya Pauni Milioni 100 kwa nia ya kuwezesha kuondoka katika miezi ijayo.

Paris Saint-Germain wamemtazama Osimhen kuhusu azma yao ya kuchukua nafasi Kylian Mbappe, lakini Gianluca Di Marzio anadai Chelsea wamejaribu kujitosa kuwania saini yake kwa kuwasiliana na SSC Napoli.

Chelsea wanatafuta njia za kuepuka kuzuia kipengele cha kuachiliwa cha Osimhen, ambacho kinapaswa kulipwa kwa ukamilifu, na wako tayari kutoa wachezaji wachache kwa SSC Napoli ili kubadilishana na huduma ya Osimhen.

Katika mpango huo wanataka kumtumia Lukaku ambaye yuko kwa mkopo kule AS Roma kwa makubaliano ambayo hayajumuishi kifungu cha ununuzi.

Chelsea wana makubaliano na Mbelgiji huyo kwamba atapatikana kwa ada ya Pauni Milioni 37 msimu huu wa majira ta joto ikiwa ni hasara ya Pauni Milioni 60.5 kwa kiwango ambacho walilipa Inter mnamo 2021.

Mpango kutoka Chelsea ni kumpeleka Lukaku SSC Napoli sambamba na ada ya kati ya Pauni Milioni 70, huku ‘The Blues’ pia wakisemekana kuwa tayari kujumuisha mchezaji chipukizi katika ofa yao ya kumpeleka Osimhen Starnford Bridge.

Nia ya SSC Napoli kumnunua Lukaku, ambaye amefunga mabao 12 katika mechi 30 za Serie A akiwa na AS Roma msimu huu 2023/24, bado haijaeleweka, ingawa mkurugenzi anayekuja wa michezo Giovanni Manna anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa Mbelgiji huyo.

Newcastle Utd kuvuruga mipango Old Trafford
Gesi kama Luku: Tafuteni Wataalamu tufanye nao kazi - Rais Samia: