Serikali nchini, imetakiwa kuendelea kudumisha na kuimarisha maadili ya Kitanzania ikiwemo kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto, kwani hali hiyo isipokemewa maendeleo yatakuwa hayana maana na ni hatari kwa mustakabali wa vizazi vijavyo.

Wito huo, umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu katika moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya na Dar24 Media kuhusu mchango wake wa Aprili 6, 2023 Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia hotuba ya Waziri Mkuu ya Mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu.

Alisema “Taifa linawekeza kwa mustakabali wa vizazi vijavyo, hivyo unahitajika umakini pasi na kukopa mila na desturi za mataifa ya nje ambayo yapo kinyume na maadili ya Kitanzania, suala hili linalohusiana na ukatili kwa watoto wetu, ulawiti na ubakaji kwa watoto wetu na maswala ya ndoa ya jinsia moja yasifumbiwe macho.”

Msambatavangu ameongeza kuwa “mambo haya tuyakemee tuyaongelee katika Nyumba za Ibada Makanisani, Misikitini na sisi tunaanza hapa bungeni, pia tuyaongelee Serikalini na kwenye Familia zetu, hizi reli zitakuja kupandwa na popo kama ilivyokuwa Sodoma na Gomora, huo umeme na majengo makubwa na barabara tunazoyajenga zitakuwa hazina maana.“

Kocha Mtibwa Sugar hajataka tamaa
Van Dijk: Nitakuwa sehemu ya mabadiliko Liverpool