Nahodha na Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk, amesema atakuwa sehemu ya mabadiliko ya klabu hiyo baada ya Kocha Jurgen Klopp, kuondoka kipindi cha majira ya joto.

Klopp alithibitisha kuondoka kwake mwezi Januari, huku uvumi ukiibuka mara moja kuhusu mustakabali wa muda mrefu wa Van Dijk katika klabu hiyo.

Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, unamalizika mwishoni mwa msimu ujao, lakini amesema ananuia kuwa sehemu ya mabadiliko ya walinzi wa Liverpool, huku Kocha wa Feyenoord, Arne Slot, akitarajiwa kuteuliwa kuchukua nafasi ya Klopp.

“Kutakuwa na mabadiliko makubwa na mimi ni sehemu ya hilo,” alisema Van Dijk.

“Nadhani klabu ina shughuli nyingi na nani atakuwa kocha mpya hilo ndilo jambo kuu. Kama nilivyosema nina furaha sana hapa, ninaipenda klabu na unaweza kuona hivyo pia.”

“Ni sehemu kubwa ya maisha yangu tayari, na hilo ndilo ninaweza kusema. Kutakuwa na mabadiliko mengi yatatokea na siwezi kusema neno la kutisha ni neno sahihi, lakini ni ya kuvutia na kusisimua sana kwa kitakachotokea.”

Klopp amebakiza mechi mbili kama kocha wa Liverpool, dhidi ya Aston Villa juma lijalo, kabla ya Wolves kuzuru Anfield siku ya mwisho ya msimu.

Van Dijk, ambaye alisajiliwa na Klopp kwa Pauni Milioni 75 Januari 2018, alikiri kuwa itakuwa fainali ya hisia siku chache chini ya Mjerumani huyo.

“Ninajivunia kumtumikia, kupigania beji na yeye na kuhesabu mafanikio tuliyopata kwa miaka mingi pia,” aliongeza Van Dijk.

“Itakuwa na hisia siku ya mwisho lakini ni sehemu ya maisha wakati mwingine. Mambo mengi yanatokea nyuma ya pazia, lakini tunazingatia siku za mechi na hilo ni jukumu letu, kazi yetu na tunataka kutimiza alama sita za mwisho.”

Serikali yashauriwa kuimarisha maadili ya Kitanzania
Serikali yapeleka somo la Kiingereza darasa la kwanza