Na Boniface Gideon, Tanga

Timu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga ambayo ilitamba miaka ya hivi karibuni kwenye Ligi kuu Tanzania Bara, Rasmi imenunuliwa na Mfanyabiashara maarufu wa Madini Wilayani Korogwe mkoani Tanga na Mkoa wa Shinyanga Ahmed Waziri Gao na sasa makao yake makuu yatakuwa mkoani Tanga.

Ikumbukwe kuwa Mwadui kwasasa imetinga hatua ya Nusu Fainali ya ligi Daraja la pili maarufu kama First League na endapo itafanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya ligi hiyo basi itakuwa imejihakikishia kupanda ligi Daraja la Kwanza maarufu kama ‘Championship’ kwa  msimu ujao 2024/25.

Mkurugenzi wa Timu hiyo Ahmed Waziri ‘Gao’ amewaeleza Waandishi wa Habari Kuwa, timu hiyo kwasasa imenunuliwa kutoka kwa wamiliki wa awali na sasa imehamia Wilayani Korogwe.

“Tumeamua kuweka nguvu kubwa ya fedha ili tuipandishe timu yetu Ligi Kuu, hivyo wadau wa soka hasa mkoani Tanga tunawaomba waisapoti, hii ni timu yao.” amesema Gao

Kuhusu kubadilisha jina la Timu hiyo, Gao amesema wapo kwenye mchakato kama wataweza kubadilisha jina lakini wanaangalia jina ambalo litaendana na Mila na Desturi za Korogwe na Mkoa wa Tanga.

“Unajua mimi ni mzaliwa wa Korogwe mkoani Tanga, nikiwa huko nina tabia za kuomba timu ili niwekeze lakini sasa hivi nimeinunua timu hii moja kwa moja tunaangalia jina ambalo litaendana na Mila na Desturi za asili yetu, Korogwe kuna Mdumange lazima tuangalie asili hiyo” amesema Gao

Kwaupande wake Kocha wa timu hiyo, Salhina Mjengwa, amesema wamejipanga kupanda Ligi Daraja la Kwanza ‘Championship’ kisha Ligi Kuu, hivyo ni lazima watwae Mataji yote wanayoshiriki, ili kufikia malengo waliojiwekea.

“Tumejipanga kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara, na tutahakikisha tunatwaa Mataji yote tunayoshiriki ili tupate fursa ya kupanda Ligi Kuu, maandalizi ya kuelekea hatua ya Nusu Fainali yamekamilika na tupo tayari kwa michezo ya hatua inayofuata” amesema Mjengwa

Wagonga nyundo kumng’oa Wesley
Newcastle Utd kuvuruga mipango Old Trafford