Baada ya kuthibitisha wataachana na Meneja wao kutoka nchini Scotland David Moyes mwishoni mwa msimu huu 2023/24, imefahamika kuwa Uongozi wa Klabu ya West Ham United umepanga kukiimarisha maradufu kikosi chao chini ya Benchi jipya la Ufundi litakalotangazwa baadae.

Gazeti la Daily Mail mapema hii leo Jumatano (Mei 08) limeripoti kuwa, Uongozi wa klabu hiyo umedhamiria kufanya hivyo, ili kuwa na kikosi imara kwa msimu ujao 2024/25.

Mchezaji wa kwanza anayetajwa kuwindwa klabu hapo kwa mujibu wa gazeti hilo ni Kinda kutoka nchini Brazil na Klabu ya Corinthians Wesley Gassova Ribeiro Teixeira ‘Wesley’.

Thamani ya Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19 inatajwa kufikia Pauni Milioni 21, lakini inadaiwa kuwa tayari Uongozi wa Corinthians umeanza kuiwekea ngumu West Ham.

Gazeti hilo limeandika: “West Ham United inajipanga kumsajili Kinda wa Klabu ya Corinthians Wesley, kama sehemu ya harakati za klabu hiyo kuimarika kikosi chake kuelekea msimu ujao 2024/25.

“Mail Sport inaelewa kuwa wawakilishi wa ‘The Hammers’ walimfuatilia Kinda huyo wakati wa mchezo wa ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu ya Brazil ‘Serie A’ mwezi uliopita ili kujiridhisha.

“Wesley, ambaye anaweza kucheza kama Kiungo Mshambuliaji ama Mshambuliaji wa Kati, thamani yake inatajwa kufikia Pauni Milioni 21 na tayari Uongozi wa Klabu ya Corinthians umeanza kuiwekea ngumu West Ham.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 9, 2024
Mwadui FC yahamia Tanga, yajipanga kurejea Ligi Kuu