Mgombea urais wa Chama cha ACT Wazalendo, Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kuboresha mfumo wa utumishi wa serikali ikiwemo kuongeza mishahara na kulipa posho stahiki kwa wafanyakazi.

Akizungumza hii leo Oktoba 12,2020 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Ditia Pemba, amesema kuwa ataongeza mshahara kutoka shilingi za Kitanzania laki tatu hadi laki tano.

”Nitaboresha utumishi na mfumo wa utumishi wa serikali pamoja na vikosi vya SMZ na tutarejesha posho zote ambazo wafanyakazi wanastahili kupewa, Mwaka wa kwanza nitakapoingia madarakani nitaongeza mshahara kutoka laki tatu hadi laki tano na hadi namaliza miaka yangu mitano kima cha chini hakitapungua laki saba na mia tano,”amesema Maalimu Seif.

mgombea huyo amewataka wananchi hao kufanya maamuzi sahihi ili kupata kiongozi ambaye atasimamia haki na kuleta maendeleo.

Chagueni madiwani wa CHADEMA- Lissu
Mafunzo kazini kuimarisha utendaji kazi wa vijana