Lydia Mollel – Morogoro.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mzava ameeleza kutoridhishwa na utaratibu uliotumika kukamilisha uboreshaji wa mradi mkubwa wa Maji wa Sofi Mission, uliopo Wilayani Malinyi baada ya kubaini kuwepo kwa uzembe wa ufatiliaji na mapungufu katika ulipaji wa kodi na matumizi ya mfumo wa manunuzi kwa njia ya kidigitali NeST.

Uboreshaji wa Mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 kwenye mnara wenye kimo cha mita sita, ufungaji wa mfumo rahisi wa kutibu maji, uboreshaji wa vituo 11 vya kuchotea majina ujenzi wa uzio kwa gharama ya shillingi 156,955,962 chini ya Mkandarasi wa Dar es Salaam.

Awali, akisoma taarifa Kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ,Meneja wa RUWASA wilaya ya Malinyi Mhandisi Marco Chongero amesema Mradi huo tayari umeanza kutoa huduma kwa wananchi

Maandamano: Lissu agusia Tume huru, Katiba mpya Babati
Arusha: Wafanyabiashara wapongeza ulinzi waomba camera