Eva Godwin – Dodoma.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika mwaka wa fedha 2024/25 imepanga kutekeleza vipaumbele vitano vyenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kuwezesha Vijana wa Kitanzania kupata maarifa, ujuzi, kujiamini, kujiajiri na kuajirika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo wakati akiwasilisha mwelekeo wa utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 na kudai kuwa vipaumbele vimejielekeza katika kutegemeza tafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu katika agenda ya maendeleo ya nchi.

Amesema, “vipaumbele vya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 ni kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini, kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.”

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Kuhusu kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya elimu ya Msingi, Sekondari na Ualimu, Mkenda amesema Serikali itawezesha ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata 226, Nyumba za Walimu wa Sekondari 184 na ununuzi wa vifaa vya Maabara.

“Pia itawezesha ujenzi wa madarasa 2,018 msingi 1,221 na sekondari 797, mabweni 114 kwa shule za sekondari, nyumba za walimu 658 msingi 567 na sekondari 81,matundu ya vyoo 2,848 msingi 1,514 na sekondari 884, Maabara 10 na vituo vya walimu TRCs 300 kwa lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji Aidha, itakamilisha ujenzi vyumba vya madarasa 111 katika shule za msingi 37, matundu ya vyoo” amesema Prof. Mkenda.

Ameongeza kuwa, “pia Maabara, Nyumba za Walimu na Mabweni katika Shule za Sekondari 50 na itaweka Nishati safi ya kupikia, ili kuendelea kuhifadhi na kuimarisha mazingira katika Vyuo vya Ualimu 11 vya Nachingwea, Katoke, Kleruu, Tabora, Dakawa, Patandi, Mpwapwa, Sumbawanga, Mhonda, Kasulu na Monduli na kununua samani kwa ajili ya Chuo cha Ualimu Sumbawanga, Mhonda, Dakawa na Ngorongoro.”

Arne Slot athibitisha kuajiriwa Liverpool FC
Wakala: Barcelona haimtendei haki Vitor Roque