Wakala wa Mshambuliaji kutoka nchini Brazil na FC Barcelona Vitor Roque, amesema haelewini kwa nini mshambuliaji huyo amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara na kupendekeza kwamba anaweza kuondoka katika majira ya joto ikiwa hali hiyo haitatatuliwa.

Roque mwenye umri wa miaka 19, aljiungaa na FC Barcelona kwa kitita cha Euro milloni 31 kutola Athletico Paranaense mwezi Januari na tangu wakati huo amefunga mabao mawill katika mechi 13 nyingi akitokea benchi.

Kinda huyo amekuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika katika mechi nne za mwisho za Barca, tatu kati yake walipoteza, na sasa wakala wake, Andre Cury amesema Roque hana furaha.

“Vitor Roque anapaswa kuwa na dakika zaidi na hakuna anayeelewa kwa nini hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara,” alisema Cury akiiambia RACI.

“(Kocha wa Barca), Xavi Hernandez hajawahi kuzungumza na mchezaji na sielewi hali hiyo. Sio nzuri kwa mtu yeyote.

“Mtoto anapaswa kufanya kazi kwa bidii na kusubiri nafasi yake, lakini tayari kumekuwa na michezo mingi ambayo angeweza kupewa dakika hizi na jukumu kubwa zaidi.

“Katika dakika 300 alizocheza, amefunga mabao mawili, ambayo inawezekana ni kiwango bora zaidi katika timu. Xavi ametoa nafasi kwa Fermin Lopez, Pau Cubarsi na Lamine Yamal, lakini si kwa Vitor Roque”

Cury pia alisisitiza kwamba ilimchukua Vinicius Junior muda kuwa mchezaji wa muhimu katika Klabu ya Real Madrid baada ya kujiunga nayo mwaka 2018, awali akiichezea timu ya akiba, lakini akasemna waandishi wa habari huko Barcelona hawampi subira kama hiyo.

“Barcelona, kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vinazungumza machafu na kusema mambo ambayo si ya kweli,” alisema Cury.

“Haisaidii. Angalia kilichotea kwa Vinicius huko Madrid. Alichukua miaka miwili na nusu kucheza mara kwa mara. Hapa Barcelona ni tofauti.”

Prof. Mkenda: Vijana kupewa maarifa ya kujiajiri, kuajirika
Malimwengu: Halima ajivunia rekodi Watoto tisa kwa mpigo