Mei 4, 2021 kulitokea tukio lililobua hisia za wengi duniani, baada ya kushuhudiwa kwa rekodi mpya iliyoandikwa jijini Casablanca nchini Morocco, ambapo Mwanamke mmoja mzaliwa wa Mali wa eneo la Kaskazini mwa mji wa Timbuktu aitwaye Halima Cisse, alijifungua watoto mapacha tisa kwa mpigo.

Katika uzao huo wa Watoto tisa wa Halima, alipata jinsia ya Wasichana watano na Wavulana wanne hali iliyopelekea kuvunja rekodi ya dunia ya kujifungua watoto mapacha, iliyokuwa ikishikiliwa na Mwanamama wa Kimarekani, Nadya Suleiman ambaye alijifungua watoto mapacha wanane mwaka 2009 wa kiume sita na wa kike wawili jijini Calfornia.

Inaarifiwa na jamaa wa karibu na familia hiyo kuwa, Mama mzazi wa Watoto hao tisa (Halima Cisse), ambaye alizaliwa Machi 21, 1996 alifurahia baada ya kujifungua watoto hao, lakini hali ilikuwa tofauti kwa baba watoto wake Arby kwani hakufurahi kabisa kupata watoto hao tisa kwa mpigo.

Halima alipata furaha hiyo ya Watoto tisa kwa uzao mmoja akiwa na umri wa miaka 25 ingawa aliwapata kwa njia ya upasuaji uliofanyika nchini Morocco, lakini kabla ya kupelekwa nchini humo Halima alilazwa katika hospitali moja iliyopo katika mji mkuu wa Mali – Bamako kwa muda wa wiki mbili hali iliyopelekea kuingia katika kitabu cha rekodi za dunia.

Wakala: Barcelona haimtendei haki Vitor Roque
Mawakala usafirishaji Wahamiaji haramu waonywa