Watu wawili (majina yao yamehifadhiwa), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, kwa tuhuma za mauaji ya Ndembora Exaud Nanyaro, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kujeruhumiwa na watuhumiwa hao mei 20, 2024  katika Kijiji cha Ngurdoto kilichopo Kata ya Maji ya chai Wilayani Arumeru.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP. Justine Masejo imeeleza kuwa marehemu alifariki dunia mei 25,2024 katika Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro, wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na watuhumiwa hao sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Masejo ameeleza kuwa, chanzo cha shambulio hilo lililopekea mauaji hayo ni ugomvi wa wanandugu na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha mauaji hayo na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.

Kufuatia tukio hilo, Polisi Mkoani humo wametoa wito kwa Wananchi kutojichukulia sheria Mkononi na baadala yake wafike katika mamlaka zinazohusika, ili kutatua changamoto zao ikiwa ni pamoja na Viongozi wa dini.

Prof. Mkenda: Watakaofaulu Sayansi, Hesabu kusomeshwa bure
MALIMWENGU: Muziki wa ajabu wasababisha majanga