Serikali Nchini, imesema utaratibu wa ajira kwa kada saidizi ikiwemo Wahasibu, Maafisa ugavi na Madereva kwasasa unafanywa na sekretarieti ya ajira na Utumishi, hivyo hazijumuishwi kwenye kada zawatumishi wa Afya kama ilivyo kwa Madaktari, Wauguzi na Wafamasia ambao utaratibu wa ajira husimamiwa na Wizara ya Afya

Hayo yamebainishwa hii leo Mei 24, 2024 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Conchesta Leonce Rwamlaza.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel.

Katika swali lake namba 436, Rwamlaza aliuliza ni kwa nini kada zinazowezesha utendaji kazi katika Hospitali hazijumuishwi pindi ajira zinapotangazwa, ambapo Dkt. Mollel alisema tayari Serikali imeweka utaratibu kwa watu wanaojitolea katika ajira kupewa kipaumbele pale ajira zinapotoka.

Amesema, “Ili kupunguza tatizo hili, tutaboresha mkakati wa mawasiliano ndani ya Serikali kwa kuonesha mahitaji halisi ya kada hizo ili vibali vya ajira vinavyotolewa vizingatie pia mahitaji ya kada husika ndani ya Wizara ya Afya.”

Inonga aukana mkataba Simba SC
Motsepe amkosoa Mwamuzi CAF