Kocha Mkuu wa Feyenoord, Arne Slot, amefichua kuwa anatarajia tangazo la hatima yake litatolewa hivi karibuni anapojiandaa kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp katika Kabu ya Liverpool ya England.

Wekundu hao Anfield walikubaliana na Slot mwezi uliopita na wakafikia makubaliano yenye thamani ya euro milioni 15 na Feyenoord ili kumwajiri bosi huyo wa Uholanzi na wasaidizi wake wachache.

Liverpool walirejea katika njia ya ushindi Jumapili (Mei 05) kwa kushinda mabao 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspur, na Slot alikiri kuwa alitazama mwanzo mwisho mchezo huo kabla ya kuwaongoza Feyenoord dhidi ya PEC Zwolle.

“Niliona dakika chache za mchezo, lakini ilibidi tuje uwanjani,” alifichua.

“Bao la kwanza tu, bao kubwa. Ulikuwa ushindi mzuri kutoka kwa Liverpool. Ikiwa uthibitisho rasmi upo, na niende huko, nitatazama michezo mingi kutoka kwao.

“Wakati mwingine maishani fursa zinakuja na lazima usikilize, nimeamua mwenyewe, siku na majuma yajayo utaona tangazo.

“Mwaka jana nilifanya chaguo la kubaki na sasa labda nilifanya chaguo lingine.”

Aliongeza: “Sina wasiwasi hata kidogo kama itaendelea swali ni lini itawasilishwa.”

Baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya PEC Zwolle, Slot alionekana akiwapungia mkono mashabiki waliokuwa kwenye jukwaa huku uso wake ukioneshwa kwenye Luninga kuzunguka uwanja, na bosi huyo wa Uholanzi alikiri ilionekana kama kwaheri.

“Nadhani nakubaliana na hilo, kwamba ilionekana hivyo,” alisema.

“Kwa sababu ya uvumi wote kwenye vyombo vya habari nadhani wanatarajia niondoke. Ndio, hilo ni jambo ambalo tunaweza kusema.”

Ten Hag: Tulistahili kipigo, mashabiki watusamehe
Prof. Mkenda: Vijana kupewa maarifa ya kujiajiri, kuajirika