Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Dorothy Semu amesema kuwa mpinzani katika siasa za Tanzania ni kuchagua fungu ambalo linanapitia kwenye changamoto nyingi, kitu ambacho anaona upo umuhimu wa kuwaelimisha Watanzania juu ya siasa za ushindani.

Doroth ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalum katika Studio za Dar24 Mediazilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na kusema, upo umuhimu wa Watanzania pia kuhafamu kwamba mawazo ya kisiasa kwa upinzani huwa yana mtizamo tofauti na chama kilicho madarakani.

Amesema, “lakini kuna uwezekano kwa wakati mmoja au mara nyingi ile mitizamo ikafanana au kuna uwezekano mara nyingi mitizamo ikatofautiana, lakini sisi kama Wanasiasa tuna wajibu wa kuilinda Tanzania kama Taifa na tunafanya kazi ili kuleta mabadiliko katika Taifa letu.”

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Dorothy Jonas Semu.

Aidha, Doroth ameongeza kuwa nafasi ya kuendesha siasa za upinzani Nchini ipo lakini watawala hawataki kukubali pale wanapoona vyama vya upinzani vinaendelea kukukua na kuonesha mafanikio, hali inayopelekea kupata alama mbaya kuwa ni CCM B, hivyo upo umuhimu wa kuendelea kujipambanua kiuafasaha, ili kuelezea makusudio yao katika jamii.

“Kwahiyo hilo silishangai sisi kama wanasiasa kama ACT – Wazalendo tutaelezea makusudio yetu katika jamii kupitia sera, mitazamo na mambo ambayo tunaona ni bora kufanyika tukiamini kwamba wale wachache ambao wamekuwa na hayo mawazo watabadilika kupitia kujipambanua kwetu kwa sera,” alisema Kiongozi huyo wa ACT.

Kuhusu nafasi aliyoachiwa na chama ambayo ameirithi kwa mtangulizi wake Zito Kabwe kwamba inazua hofu huenda asiitendee haki, Doroth amesema ni kweli viatu vyake ni vikubwa kutokana na ukongwe wake kisiasa, lakini anajiamini na nafasi aliyonayo ameigombea baada ya kujipima, hivyo ataendelea kuitetea kwa kutekeleza majukumu yake kiufasaha.

Kinda la kibrazil latajwa Old Trafford
Ten Hag: Tulistahili kipigo, mashabiki watusamehe