Gwiji wa Soka nchini Ufaransa Marcel Desailly amemuonya Zinedine Zidane kuhusu mpango wa kuchukua kazi ya kukinoa kikosi cha FC Bayern Munich.

Zidane anatajwa kupewa kipaumbele cha kuchukuwa nafasi ya kuliongoza Benchi la Ufundi la Klabu hiyo ya mjini Munich, ambalo kwa sasa linaongozwa na Thomas Tuchel atakayeondoka mwishoni mwa msimu huu.

Desailly ameiambia Sport1 kuwa Zidane anapswa kuwa makini endapo mpango wa kupewa nafasi ya kuwa kocha mkuu FC Bayern Munich utafanikiwa kama inavyotajwa katika vyombo kadhaa vya habari nchini Ujerumani.

Amesema Kocha huyo ambaye alicheza naye kwenye kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 1998, anapaswa kuwa makini katika usajili wa wachezaji na kuwaondoa baadhi ambao kwa sasa hawana msaada kwenye klabu ya FC Bayern Munich.

“FC Bayern Munich ina wachezaji wachache wanaozoea falsafa ya Zidane na 4-3-3 yake. Klabu inapaswa kutumia pesa nyingi kurekebisha timu na kuibadilisha kulingana na mahitaji yake.

“Lakini kwa nini usifanye hivyo? Ikiwa Bayern kweli wanataka mabadiliko makubwa hii itakuwa fursa sahihi. Lakini hii itategemea na usajilia takaoufanya na kuwaacha baadhi ya wachezajia mbao wanaonekana hawana msaada.”

Wakati huo huo Desailly pia amesema kuhusu Kingsley Coman kuwa na uwezekano wa kuziwahi Fainali za mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’: “Itakuwa ngumu kwake kuwa kwenye Mashindano ya Uropa.

“Baada ya jeraha, hata hivyo, lazima aimarike kimwili na kutafuta njia yake na jukumu linalomfaa zaidi.”

Engikaret: Waliojichukulia sheria mkononi kusakwa
Mafuriko yauwa 13, Wananchi watakiwa kuhama mabondeni