Lydia Mollel – Morogoro. 

Jeshi la Polisi Nchini limekusudia kugawa vifaa vya kusaidia Wanafunzi  kuvuka barabara kwa Wanafunzi wa shule zote zilizopo pembezoni mwa barabara.

Akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwere iliyopo Manispaa ya Morogoro, Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Michael Deleli amesema mbali na kuwagawia vifaa hivyo, pia watawapa elimu namna ya kuvitumia ili kujihakikishia usalama wao wakati wa kuvuka barabara.

Aidha, ACP Deleli, ametoa elimu kwa abiria wa mabasi katika Kituo cha mabasi yaendayo Mikoani cha Msamvu, ili kujua wajibu wao kama abiria na kuwataka madereva na makondakta kuacha kupakiza mizigo hatarishi ya milipuko na mikaa.

Huduma za kibingwa: Tanganyika yapokea Madaktari wengine 17
Rufiji: Mashamba yaliyoathiriwa na mafuriko yatengewa Mamilioni