Lydia Mollel – Morogoro.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro leo Mei 4, 2024, ameongoza hamasa ya kucheza mchezo wa Gofu kwa madiwani wa Manispaaa ya Morogoro kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya mchezo huo huku akitoa wito kwa jamii kushiriki kucheza mchezo huo.

Akizungumza wakati wa hamasa hiyo mkoani Morogoro  Dkt. Ndumbaro, amesema kuwa ni wajibu wa kila mwana Morogoro kutunza miundombinu ya michezo ukiwemo uwanja Gofu Gymkhana uliopo mkoani humo.

“Wito wangu kwa Watanzania wote tupende michezo na mchezo wa gofu ni mmoja kati ya michezo ambayo haichagui umri mtu yeyote anaweza kucheza” Amesema MNdumbaro

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ameitaka jamii kuacha dhana ya kufikiri kuwa mchezo wa Gofu ni wa watu wenye kipato cha juu badala yake wajifunze mchezo huo kwa kuwa una manufaa makubwa.

 

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 5, 2024
Huduma za kibingwa: Tanganyika yapokea Madaktari wengine 17