Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwassa amewataka watumishi wa umma ndani ya Mkoa huo kutazama mafao yao kama yanapelekwa kwenye mfuko husika na kujua wameweka kiasi gani na kwamba jambo hilo liwe jukumu la watumishi wote wa Serikali kabla ya muda wao wa kustaafu.

Mwassa ametoa kauli hiyo wakati akihutubia watumishi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya mei mosi kimkoa zilizofanyika katika viwanja vya Kaitaba vilivyopo manispaa ya Bukoba.

Amesema, “usipo fatilia mafao yako mapema kabla ya kustafu baadae itakuwa changamoto kubwa maana baadae miguu itakuwa haiwezi kutembea utakuwa unanyata na nauli haipo ya kutosha nawaomba mfanye hayo sasa watumishi wenzangu.”

Katika hatua nyingine, Mwassa, amesema Serikali itahakikisha inasimia mifuko yote ya jamii mkoani humo, itoe mafao ya wastaafu kwa wakati, ili yaweze kuwanufaisha wahusika.

Awali, akisoma risala Kwa niaba ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi mkoa humo Katibu wa Chama cha Walimu – CWT Kagera, Njile Lufansiza amesema wanatambua mchango wa serikali kwa uhitaji wa ajira na kupandishwa madaraja na kuomba serikali kutazama upya Sheria ya kikokotoo na kupandisha mishahara kwani changamoto hizo zimefanya watumishi wengi kuishi maisha magumu.

Ulega awafariji waathirika wa mafuriko Mkuranga
Majaliwa: Wakandarasi Miradi ya umwagiliaji wazingatie ubora