Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewatembelea na kuwafariji wananchi waliothiriwa na mafuriko katika Kata za Kisiju na Shungubweni, Wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.

Akitoa salamu za pole, Ulega amesema Rais Samia amemtuma kuwafikishia wananchi hao salamu zake za pole pamoja na chakula, magodoro na vifaa vingine vya ndani ili viwasaidie katika kipindi hiki wakati serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi hao wanarejea katika maisha yao ya kawaida.

Sehemu kubwa ya wananchi hao ambao Ulega amewatembelea nyumba zao zimeathiriwa kwa kuzingirwa na maji na kupelekea kukosa makazi na hivyo kulazimika kukaa katika makambi.

Jumla ya vitu ambavyo Mbunge huyo amekabidhi kwa niaba ya Rais Samia ni Mchele tani 4, Unga tani 5 na Maharagwe tani 10 ambavyo amekabidhi kwa Vijiji vya Kerekese, Kalole, Mavunja na Kisiju Pwani.

Serikali yajipanga kuimarisha uzalishaji mbegu bora
Mwasa: Fuatilieni mafao yenu yanapelekwa wapi