Serikali kupitia Wizara ya kilimo katika mwaka 2023/2024 imejipanga kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora nchini kwa kuendelea kuiwezesha ASA kujenga na kukamilisha miundombinu ya umwagiliaji yenye jumla ya hekta 3,304.8 ifikapo mwaka 2025 katika mashamba yote ya mbegu.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameyasema hayo hii leo Mei 2, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara ya kilimo na kuongeza kuwa mashamba ni kilimo (hekta 300), Msimba (hekta 400), Bugaga (hekta 100), Mbozi (hekta 400), Luhafwe (hekta 400), Dabaga (hekta 300), Namtumbo (hekta 500), Arusha (hekta 100), Kilangali (hekta 300), Mazizi (hekta 4.8), Msungura (hekta 100) na Mwele (hekta 400).

Amesema, “na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji wa hekta 220 kati ya 400 katika shamba la Kilimi umekamilika,na ukamilishaji wa eneo la hekta 180 katika shamba hilo unaendelea.”

“Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Arusha hekta 200 umefikia asilimia 55,Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika Shamba la Msimba hekta 200 umefikia asilimia 45, Ujenzi wa bwawa lenye ujazo wa lita milioni 45 katika shamba la mbegu Arusha umekamilika, Ujenzi wa bwawa lenye ujazo wa lita milioni 45 katika shamba la Msimba umefikia asilimia 70 na uwekezaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa njia ya matone katika shamba la Tengeru lenye ukubwa wa hekta 5.5 umekamilika,” amesema Bashe

Hata hivyo, amesema Wizara imepanga kuiwezesha ASA kujenga ghala katika mashamba ya Arusha, Mbozi, Namtumbo, Msungura na Kilangali na kuongeza kuwa, “katika kujenga ghala tulipanga kununua na kufunga mitambo miwili (2) ya kuchakata mbegu katika mashamba ya mbegu ya Mbozi na Namtumbo na kulipa fidia ya mashamba mapya ya mbegu ya Tanganyika (Luhafwe), Namtumbo na Chalinze (Msungura na Mazizi).”

“Hadi Aprili, 2024 taratibu za manunuzi ya wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa ghala la Arusha zimefikia hatua ya kusaini mkataba na mshauri elekezi, aidha, taratibu za ununuzi wa mitambo miwili (2) ya kuchakata mbegu katika mashamba ya mbegu ya Mbozi na Namtumbo,” amesema.

Tanganyika: Wahanga wa mafuriko wapatiwa maeneo
Ulega awafariji waathirika wa mafuriko Mkuranga