Johansen Buberwa – Kagera.

Katika kuadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera imekusanya Unit 51 za Damu salama kutoka kwa wadau mbalimbali.

Akizungumza na Vyombo vya Habari, Mratibu wa Damu Salama Manispaa ya Bukoba, Justine James amesema zoezi hilo limefanikishwa na watu waliohudhuria maadhimisho hayo na  zitasaidia kuimarisha afya ya Watanzania wenye uhitaji wa damu.

Amesema, “kulingana na matumizi yetu kwa wiki maana tunatumia uniti 75 na kwa mwezi tunahitaji unit 300 na kwa mwaka uniti 3600 kwahiyo tunashukuru sana kwa wote walioshiriki katika zoezi hili akiwemo Mkuu wetu wa Wilaya aliyeongoza uchangiaji huo.”

Naye Mwanafunzi wa kidato cha sita na Kiongozi wa Damu salama wa Shule ya Sekondari Kahororo, Kelvin Edwini amewaomba Vijana kuchagia damu salama kama yeye alivyofanya hii leo kwani hitaji hilo haliwezi patikana sehemu yoyote isipokuwa kwa Watanznia ili kunusuru afya za wenye uhitaji.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Bukoba Mjini, Daniel Muhina amesema amemeamua kushiriki katika zoezi la uchangiaji Damu salama ili kuokoa roho za Watanzania wengi na kwenye maadhimisho ya Muungano Rais kupitia Hotuba yake aliwaelekeza kushiriki, hivyo wametekeleza.

Katika hatua nuingine Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima ametoa wito kwa wananchi wanaoshi ndani ya Wilaya hiyo kuendelea kuuenzi Muungano kwa kufanya kazi na kushiriki katika huduma za kijamii.

Arusha: Wafanyabiashara wapongeza ulinzi waomba camera
DC Buswelu: Tuuenzi Muungano kwa kufanya kazi halali