Swaum Katambo, Katavi.

Baraza Kuu la Waislam Tanzania – BAKWATA, Mkoa wa Katavi limezindua mfumo wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli mbalimbali za kiofisi, uliogharimu zaidi ya shillingi milioni 2.5

Katavi, unakuwa mkoa wa kwanza nchini kuanza kuutumia mfumo huo tangu kuzinduliwa na mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir.

Akizindua mfumo hu, Meneja wa Benki ya TCB, Chacha Petri amepongeza hatua hiyo ya BAKWATA kuingia kwenye matumizi ya TEHEMA na kueleza kuwa huo ndio mfumo wa kisasa ambao taasisi makini inapaswa kuutumia.

Katika hatua nyingine Chacha ameahidi kutoa vifaa ikiwemo kamera na kompyuta mpakato (laptop) kwa BAKWATA Mkoa wa Katavi kama moja ya njia ya kuendalea kuimarisha matumizi ya TEHAMA kwa taasisi hiyo.

Sheikh wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Kakulukulu amesema mfumo wa TEHAMA ni moja kati ya hatua za mabadiliko ndani ya BAKWATA chini ya mufti mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir wa kutaka wailam kutoachwa nyuma na Teknolojia.

Uzinduzi wa mfumo huo umejumuisha ugawaji wa vishikwambi vinne (4) ambavyo vitasaidia kuendesha mfumo wa TEHAMA katika ofisi ya BAKWATA mkoa wa Katavi, Ofisi 3 za BAKWATA Wilaya za Mpanda, Tanganyika na Mlele na Printa moja kwa ajili ya ofisi ya Mkoa.

 

DC Buswelu: Tuuenzi Muungano kwa kufanya kazi halali
MALIMWENGU: Tangazo kodi ya wafuga ndevu lazua tafrani