Ama kweli mambo ni mengi duniani sema muda tu ndio tatizo, eti leo tunachukua muda wetu, ili kujadili jambo ambalo ni la kihistoria linalopaswa kujulikana na kila Mwanamume, kila Mwanamke na kila Mtoto kwa kitendo cha kudharauliwa na cha kufedhehesha kwa Wanaume wote ulimwenguni, tena kikifanywa na Mwanaume mwenzetu.

Mwaka 1535, Mfamle Henry VIII wa Nchini Uingereza aliibua mjadala uliowashtua watu kwa kutoa tangazo la ushuru kwa Wanaume wote waliochagua kufuga ndevu zao lililojulikana kama ‘kodi ya ndevu’.

Labda katika jitihada za kuondoa ushindani katika medani ya ndevu, Henry VIII aliweka ushuru wa kimaendeleo kwa wale Wanaume wale ambao waliochagua kusimama kinyume na mapenzi yake na kuendelea kufuga ndevu zao.

 

Kwa hiyo, badala ya kudhani anaharibu mtindo wa nywele za sharafa, Mfalme huyo wa Uingereza bila kujua, alizipa ndevu na mtindo huo hadhi, hali iliyopelekea matajiri wengi kumudu kuzifuga na kuzilipia hali masikini wakiwaheshimu wafuga ndevu na wao kushindwa kuzifuga kwa kukosa kodi.

Kwa njia fulani iliyowachanganya watu, baadhi yao waliiona kuwa ni sera ya kiuchumi ya Henry VIII isiyo na upeo wa kushukuru kwa kuenea kwake, badala ya uhaba wa ndevu katika jamii ya kisasa yenye Wanaume marijali, Henry alitukosea sana sisi masikinip.

Na kwa kuthibitisha hili Wanaume wengine waliamua kutoa matusi na kejeli kwamba Henry VIII mwenyewe, alikuwa anafuga hizo ndevu wakati wa utawala wake lakini wakahoji je? yeye alikuwa akilipa kodi wapi maana hawakuwahi kusikia wala kumuona.

Hili pia lilimkera binti yake ambaye alionekana kuchoshwa na habari za ndevu kama za baba yake zinazolipiwa kodi, hapo alichagua kutoza kodi kama hiyo ya ndevu, ili kulipwa na Mwanamume yeyote ambaye angetaka kumchumbia na kumuoa akilenga kuona nini baba yake angefanya katika hilo, lakiji Mfalme huyo hakujali.

Si ‘mnajuaga lakini’ waigaji wa mambo yasiyofaa na hata yale ya kipuuzi wapo wengi duniani, kwani zaidi ya karne moja na nusu baadaye, mwaka wa 1698, Maliki Peter I wa Urusi alitoza ushuru wa ndevu sawa na huo kwa wafugaji wa sharafa nchini mwake.

Alisema hizo ni jitihada za kuifanya milki yake kuwa ya kisasa zaidi (ambayo kwa wazi alimaanisha kunyoa nywele safi), Peter I alikusudia kutoza ushuru si tu dhidi ya watu wote wenye ndevu chini ya utawala wake, bali pia kudai kwamba wanaume hao walipaswa kuiga unyoaji wake wa ndevu.

 

Sema nini ndugu zangu, wajinga na waovu ni watu muhimu sana, huwa wanatufanya tugundue mambo mengi sana ya kuyaepuka na kuyakwepa na yasilete madhara zaidi, lakini me binafsi siwakubali wajinga wala waovu maana ‘wanaletaga’ taharuki na mijadala isiyo na msingi, kifupi wanatupotezeaga muda.

Ipo hivi, Henry I akatengeneza sarafu ya shaba iliyoundwa mahsusi kumuaibisha mtu mwenye ndevu iliyokuwa na ndege Tai wa Kirusi upande mmoja na kwa upande mwingime ilionesha nusu ya chini ya uso wa mtu mwenye pua, masharubu, mdomo na ndevu.

Kulikuwa na vifungu viwili vilivyoandikwa kwenye sarafu, kimoja kikisomeka “Kodi ya ndevu imechukuliwa” na kingine kisichofanya kazi vizuri na cha chuki zaidi, kikisomeka, “Ndevu ni mzigo mkubwa.”

Henry hakuwa na adabu kabisa yani, kwani Ndevu ni mzigo eti? …. mimi binafsi napinga aina yoyote ya kodi ya ndevu na kama wanaume wote chini ya utawala wa Henry VIII, Elizabeth I na Peter I ambao walinyoa ndevu zao, ili tu kukidhi fikra za watawala kama hao me siwaungi mkono, ila wapumzike kwa amani malijendi wote ambao hawakuunga mkono juhudi.

Kwa nyie ‘majunia’ ambao mnaoendelea kuzifuga ndevu na mnazipenda kiasi mnahisi ndio mpango mzima kama ilivyo kwa Byser, wito wangu kwenu ni kwamba, endeleeni kuzipenda ndevu zenu na mzifurahie. Ndevu ni suna jamani kazeni mtatoboa.

BAKWATA Katavi wazindua mfumo matumizi ya Tehama
Safari za Mwendokasi Mkwajuni, Jangwani zasitishwa