Njia ya Mabasi yaendayo kwa haraka ipitayo Jangwani na ile ya Kinondoni Mkwajuni zimefungwa kutokana na mafuriko yanayosababishwa na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Uongozi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka – DART, ambayo imeeleza kuwa huduma za njia mlishi kwa maeneo yasiyo na adha hiyo zitaendelea.

Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa safari ya Mabasi yanayotokea Kimara kuelekea Kivukoni, Gerezani na Morocco itaishia Magomeni Mapipa.

Kwa mabasi yanayotoa Huduma Katikati ya Jiji kwa njia ya Muhimbili na Gerezani yenyewe yataendelea na Huduma kama kawaida.

 

MALIMWENGU: Tangazo kodi ya wafuga ndevu lazua tafrani
Rufiji: Wahojiwa kwa kuficha Chakula cha msaada