Mtendaji wa Kata na Mtendaji wa Kijiji pamoja na Vijana tisa waliokuwa wabeba mizigo wanahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU wakidaiwa kuficha chakula cha waathiriwa wa mafuriko Rufiji na Kibiti kwa utaratibu usio rasmi.

Tukio hilo, limethibitishwa na Mkuu wa wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowelle ambaye alisema wahusisha Mtendaji mmoja wa kata na Mtendaji wa kijiji wametajwa na endapo wakibainika watachukuliwa hatua.

Amesema, “hizi ni taarifa za awali ila kwa haraka haraka kuna mifuko zaidi ya 20 ilidaiwa kufichwa, tulivyobaini tuliwaagiza warejeshe vyakula walivyoficha kisha kuwaripoti katika vyombo vya kisheria na kuwachukulia hatua,moja wapo kuhojiwa na TAKUKURU na baada ya uchunguzi watatoa taarifa ya kina.”

Rufiji ni miongoni mwa Wilaya iliyoathirika na mafuriko, ikiwa ji Kati ya wilaya zilizopo kwenye mikoa 14 iliyokumbwa na changamoto hiyo na tayari mwitikio wa utiaji misaada unaendelea kwa makundi mbalimbali.

Safari za Mwendokasi Mkwajuni, Jangwani zasitishwa
Miaka 60 ya Muungano: Sauti imesikika, kazi inaendelea