Lydia Mollel – Morogoro.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazohusisha utekwaji wa watoto 12 wa shule ya awali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Nchini – KKKT, Mahenge Wilayani Ulanga.

Akizungumza na Dar24 Media hii leo Mei 8, 2024 Kamanda Mkama amesema taarifa hiyo inadai kuwa watoto hao walitekwa na m

Mwanamke mmoja na kuwapakia kwenye gari na kkwamba hata hivyo alikamatwa na Polisi, jambo ambalo si kweli.

“Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro linakanusha taarifa hii na kwamba hakuna mtoto yeyote  aliyetekwa katika shule hiyo na wala mwanamke aliyekamatwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.”

“Kwahiyo tumefanya uchunguzi na ufuatiliaji wa kutosha ikiwa ni pamoja na kufika kwenye shule husika na kuongea na uongozi wa hiyo shule hata wenyewe wamekiri tukio hilo alikuwepo,” alisema Kamanda Mkama.

Hata hivyo, amewataka Wananchi wapuuze taarifa hizo kwani wameshaonana na wazazi wa watoto hao na wamekiri kuwa watoto wao na wako salama.

Aidha, Jeshi la Polisi pia limewataka wananchi kuacha tabia ya kutuma taarifa za kuzusha, na kwasasa wanaendelea na uchunguzi lakini pia wanamtafuta muhusika aliyesambaza taarifa hiyo kwenye mitandao ya kijamii ambayo imezua taharuki.

Tuchel akanusha kuombwa kubaki Bayern
TANNA yaanza maadhimisho miaka 51 ya uuguzi