Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi wa CCM Taifa, Fadhil Maganya amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni mfariji Mkuu kwani amekuwa wa  kwanza kutoa misaada ya faraja kwa waathirika wa matukio mbalimbali nchini, ikiwemo waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji kwa Wilaya za Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Maganya aneyasema hayo akiwa kwenye Kambi ya Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji huko Chumbi B wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku moja kujionea athari za mafuriko hayo na kupeleka misaada ya vyakula, mavazi na magodoro kwa waathirika hao.

Amesema, “alikuwa wa kwanza binafsi bila serikali akaleta tani 300 ambazo ni tani 100 za maharage, tani 100 za unga na tani 100 za mchele ili nyinyi Wananchi muweze kujikimu na kuondokana adha mliyokuwa mnaipata ya njaa kutokana na mafuriko hayo.”

Maganya ameongeza kuwa, Serikali imetenga maeneo kwaajili ya Waathirika hao wa mafuriko ya Mto Rufiji ili wahame kabisa mabondeni na maeneo hatarishi ya Mto huo ili wasogee maeneo salama hivyo amewataka kukubali agizo hilo.

Katika hatua nyingine Maganya aliwataka Watanzania kupuuzia upotoshaji wa taarifa za Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julias Kambarage Nyerere unaofanywa na baadhi ya watu ambapo ukweli ni kwamba Mafuriko katika Wilaya hizo yamekuwa yakitokea kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Misaada aliyoitoa Maganya ni pamoja na magodoro 30, sabuni za unga viloba 19, vyandarua balontano, mablanketi mabalo mbili, nguo za watoto, akinamama na nguo za wanaume, sahani 240, ndala dazani mbili, mikate 500, kilo 750 za sukari, unga viloba 200.

Kwa upande wake Mjumbe Baraza Kuu Wazazi Taifa (Bara), Ally Mandai alisema tayari serikali imetenga zaidi ya bilioni 66 kwa ajili ya kufanyia ukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na maji ya mvua yanarudishwa kwa haraka.

Kamati ya uongozi yaridhishwa usimamizi wa mradi JNHPP
Wizi: 11 washikiliwa kwa mahojiano, wamo watendaji wa Serikali