Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Julius Nyerere ulio chini ya Mwenyekiti Mhandisi Cyprian Luhemeja ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira wametembelea Bwawa la kufua umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) katika mto Rufiji kwa lengo la kujionea maendeleo ya Mradi huo unaotarajia kuzalisha Megawati 2115 za umeme

Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Luhemeja, walitembelea mradi huo Aprili 27,2024 ambapo katika ziara hiyo waliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio.

Baada ya Kutembelea Bwawa la Julius Nyerere Mhandisi Cyprian alisema wamefurahishwa na namna wataalamu wa Kitaanzania walivyoweza kusimamia mradi huo kwa ustadi mkubwa.

Amewasisitiza wataalamu wanaotekeleza mradi huo kuwa watanzania wanahitaji kupata huduma ya umeme wa uhakika.

“Najuwa kazi kubwa imefanyika na serikali imewekeza fedha nyingi hivyo watanzania wanatarajia kupata umeme wa uhakika muda si mrefu,” alisema.

Aidha, aliwapongeza Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme ( TANESCO) na wadau wengine kwa kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufasaha.

Mrwara: Mapokezi ya Jokate yatikisa
Jumuiya ya Wazazi CCM wakabidhi misaada Rufiji