Serikali kupitia Wizara ya Madini, inakusudia kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini, kuwawezesha upatikanaji wa mikopo nafuu na fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde hii leo Mei 9, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Dkt. Christine Ishengoma aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga.

Amesema, mpango wa Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wa Wilaya ya Ulanga ukihusisha masuala mbalimbali ikiwemo kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali, ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo.

“Mhe. Spika maeneo mengine ni utoaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo; kutoa elimu ya matumzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija; huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),” amesema Waziri Mavunde.

Kocha Pamba jiji ataka fungu la usajili
ACT-Wazalendo: Sio Zitto tu, hatuna uwezo kwa yeyote