Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amesema kama angezungumza moto ungeweka baada ya kubishana na kocha wake Jurgen Klopp kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Ham kwenye Ligi Kuu ya England juzi Jumamosi (Aprili 27).

Salah alionekana akizozana na Klopp wakati akijiandaa kuingia dakika ya 79 akitokea benchi.

Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Misri alisema hawezi kuweka wazi mabishano yao lakini mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Peter Crouch alisema mzozo huo si jambo zuri kwa klabu hiyo.

“Salah ni mchezaji aliyeanza kwenye mechi nyingi za Liverpool na atakuwa amekasirika kuwekwa benchi,” alisema Crouch.

Young Africans yaundiwa mkakati mzito Afrika

“Hakuna mtu anayependa kuona ugomvi kati ya kocha na mchezaji mwandamizi.”

Salah alionekana kuchukizwa na jambo fulani Klopp alilomwambia wakati akijiandaa kuingia kwenye mchezo huo na alionekana kutaka kuendeleza ugumvi huo kabla ya wachezaji wenzake Darwin Nunez na Joe Gomez kuingilia kati na kuwatenganisha.

Matokeo ya mchezo huo yameiondoa Liverpool kwenye mbio za ubingwa na watahitaji Arsenal na Manchester City kupoteza mechi zao kuwa na nafasi.

Katavi: Wafanyabiashara washindwa kulipa kodi
Young Africans yaundiwa mkakati mzito Afrika