Swaum Katambo, Katavi.

Asilimia 55 ya wafanyabiashara wapatao 12,000 waliosajiliwa mkoani Katavi wamebainika kushindwa kutoa risiti za kielektroniki pindi wafanyapo mauzo hali inayoelezwa kusababishwa na ukosefu wa elimu ya mlipakodi.

Hayo yamebainika katika kampeni ya mlango kwa mlango inayofanywa na mamlaka ya mapatao Tanzania (TRA) Mkoa wa Katavi yenye lengo la kutoa elimu kwa mlipakodi.

Akizungumza Meneja wa TRA Mkoa wa Katavi, Nicolaus Migera amesema dhumuni la kampeni hiyo ni kutoa elimu mlango kwa mlango kwa mkoa mzima ili kutoa elimu kwa walipa kodi wote na kufahamu changamoto zao, kuzitathmini, kuzichambua na kuona namna ya kuzitatua”amesema

Amesema kuwa utoaji wa risiti za kielektroniki hauridhishi kwa mujibu wa taarifa ya mwezi machi mwaka huu ambapo amesema ni asilimia 45 tuu ya wafanyabiashara ndio wenye uwezo wa kutoa risiti za kielektroniki.

Kwa upande wao wafanyabiashara mkoani Katavi wameiomba mamlaka ya mapatao Tanzania kuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya mlipakodi mara kwa mara kutokana na ongezeko la wafanyabiashara wapya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amewataka TRA Katavi kutatua changamoto zote zilizowasilishwa kupitia mwenyekiti wa wafanyabiashara huku akiwataka wafanyabiashara pia kulipia kodi pasipo kushurutishwa.

Aidha pia amewataka wafanyabiashara kuitumia vizuri elimu watakayopatiwa kwani kulipa kodi ni moja ya kuichangia Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya mbalimbali ya maendeleo.

Solskjaer kujaribu soka la kimataifa
Mohameed Salah: Ukimya wangu una maana kubwa