Mshambuliaji kutoka nchini Misri Mohamed Salah ameonesha nia ya kutaka kubaki Liverpool, licha kuhusishwa na mpango wa kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Mshambukliaji huyo amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia nchini Saudi Arabia, na ilielezwa mwanzoni mwa msimu wa 2023/24 alikaribia kujiunga na moja ya klabu zinazocheza Ligi ya nchi hiyo, ambayo inaendelea kujizolea umaarufu kwa sasa.

Salah amechapisha ujumbe katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa X, ambao umeonesha bado anahitaji kusalia Liverpool angalau kwa msimu mmoja.

Hata hivyo hamu ya Salah kuhitaji kubaki Liverpool, inatokana na kutaka kufanya kazi na Kocha Mkuu mpya wa klabu hiyo Arne Slot, ambaye amekabidhiwa mikoba ya Kocha Jurgen Klopp aliyemaliza mkataba wake juzi Jumapili (Mei 19).

Salah ameandika: “Tunajua kwamba mataji ndiyo muhimu na tutafanya kila tuwezalo kufanikisha hilo msimu ujao. Mashabiki wetu wanastahili na tutapigana hili kwa maslahi ya klabu yetu.”

Pia Mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 31, amemuaga Kocha aliyeondoka Jurgen Klopp, akiandika: “Ulikuwa wakati mzuri kufanya kazi na wewe, tumefanikiwa pamoja kwa kutwaa mataji yenye hadhi kubwa kwa miaka 7 iliyopita. Nakutakia mafanikio mema kwa siku zijazo na natumai tutakutana tena.”

MAKALA: Siri za ushujaa, kifo cha Rais wa Iran
Pauni Milioni 25 kumng’oa Chalobah