Mshambuliaji wa Newcastle United na Sweden, Alexander Isak huenda akalazimisha kuondoka mwisho wa msimu huu kutokana na kipengele kilichopo katika mkataba wake kinachomtaka akatwe asilimia 20 ikiwa timu hiyo itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Kwa mechi zilizobakia Newcastle haitoweza kumaliza nafasi nne za juu na kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, hivyo akiendelea kuwepo italazimika akatwe tu mshahara wake.

Hii inakuwa ni habari nzuri kwa Arsenal na Barcelona ambazo ni miongoni mwa timu zilizohitaji saini yake tangu Januari mwaka huu.

Arsenal ndio inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumpata kwa sababu Newcastle itahitaji walau Pauni 70 milioni ili kumuuza kiasi ambacho kitakuwa ni ngumu kwa Barca kukitoa kwa sasa kutokana na hali ya uchumi wao.

Tangu kuanza kwa msimu huu Isak mwenye umri wa miaka 24, amecheza mechi 35 za michuano yote na kufunga mabao 21.

Sheikh Mkuu awaombea mema waathiriwa wa mafuriko
Fumbo zito kwa washambuliaji Taifa Stars