Wachezaji watatu wa klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, wametajwa kwenye orodha ya wanaowania tuzo za msimu wa 2019/20, ambao rasmi ulifikia ukingoni mwishoni mwa juma lililopita kwa mchezo wa Fainali, Kombe La Shirikisho (ASFC).
Wachezaji hao kutoka Simba SC ni Cletous Chama, Luis Miquissone na Aishi Manula.
TFF kupitia kamati ya Tuzo imetoa orodha ya wachezaji 15 watakaowania Tuzo za msimu wa 2019/20, wakichujwa kutoka wachezaji 30 waliotangazwa mwishoni mwa juma lililopita.
Katika kinya’anyiro cha Mchezaji Bora wamo Nicolas Wadada (Azam FC), Chama (Simba) na Bakari Mwamnyeto (Coastal Union).
Wanaowania kipengele cha goli bora ni (Sadallah Lipangile) KMC vs Mtibwa Sugar, (Luis) Simba vs Alliance FC na (Patson Shikala) Mbeya City vs JKT Tanzania.
Mchezaji Bora chipukizi ni Kelvin Kijiri (KMC FC), Dickosn Job (Mtibwa Sugar) na Novatus Dismas (Biashara United)
Kipa Bora ni Daniel Mgore (Biashara United), Nourdine Balora (Namungo FC) na Manula (Simba). imu yenye nidhamu ni Coastal Uniion, Kagera Sugara na Mwadui FC huku Mwamuzi Bora ni Ahmed Arajiga (Manyara), Ramadhan Kayoko (Dar es Salaam) na Abdallah Mwinyimkuu (Singida).
Mwamuzi Bora msaidizi ni Frank Komba (Dar es Salaam), Abdulaziz Ally (Arusha) na Hamdan Said (Mtwara).
Hafla ya kutangazwa kwa washindi wa Tuzo msimu wa 2019/20 imepangwa kufanyika Agosti 7, 2020 kwenye Ukumbi wa Milimani City, jijini Dar es Salaam.