Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania ‘TaifaStars’ Hemed Morocco leo ametangaza majina ya wachezaji watakaoingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Morocco amesema kikosi kitaingia kambini Octoba 1 tayari kuanza mazoezi ya kujiwinda na mechi hiyo itakayopigwa Octoba 7 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa Stars ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.

Walioitwa kwenye timu ya taifa kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa Malawi ni wachezaji wafuatao;

Makipa:

Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) Said Mohamed (Mtibwa Sugar)

Mabeki:

Shomari Kapombe (Azam FC), Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba SC), Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Haroub (Yanga SC)

Viungo:

Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Farid Mussa (Azam FC) Salum Telela, Deus Kaseke Simon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba SC)

Washambuliaji:

John Bocco (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-Congo DRC), Mrisho Ngassa (Free State Stars-Afrika Kusini).

Lowassa Aing’ang’ania CCM, ‘Ni Shida!’
Mancini: Kufungwa Ni Jambo La Kawaida