Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA, inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia hii leo Jumatano, Oktoba 4, 2023, ambapo bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Shilingi 3,281 kwa lita ya Petroli, Shilingi 3,448 kwa lita ya Diseli na Shilingi 2,943 kwa lita ya Mafuta ya Taa.
Kwa mujibu wa Taarifa ilitolewa na Mamlaka hiyo, imeeleza kuwa mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Oktoba 2023 yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi kufikia asilimia 4.21 na gharama za uagizaji wa mafuta hadi kufikia asilimia 17 kwa petroli, asilimia 62 kwa dizeli na asilimia 4 kwa mafuta ya taa.
Aidha, sababu nyingine ni uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani – OPEC+, kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa na mataifa ya magharibi ambapo
Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali.
Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zilizoainishwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka agizo la Mamlaka huku wakikumbushwa kuzingatiz uuzaji wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja kama ilivyoamriwa.
Kupata mjumuisha wa Bei halisi na eneo kwa kila Mkoa nchini tazama Jedwali hapa chini.