Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini – TARURA, Mkoani Kagera kwa kipindi cha miaka mitatu wamefankiwa kufungua Barabara mpya takriban Kilomita 835 na kuongeza mtandao wa Barabara za changarawe kutoka kilomita 830 hadi kilomita 1858, madaraja 11, karavati 110 hali ambayo imeonekana kuwa msaada mkubwa kwa jamii hasa waishio vijijini.

Akizungumza na Vyombo vya Habari, Meneja TARURA Mkoa Kagera, Mhandisi Avith Theodory amesema kwasasa hali ya Barabara Vijijini imeendelea kuwa vizuri tofauti na awali kwani baadhi ya maeneo walilazimika kutumia mitumbwi wakati wa kusafiri lakini kwa sasa wameboreshewa na kuwekewa madaraja pamoja na makaravati.

Amesema, “kwa mfano Wilaya Kyerwa kuna eneo la Kishanda B barabara inaunganisha kata tano eneo ni tingatinga na ziwa dogo karibia mita 200 watu walikuwa wakivuka kwa mitumbwi hasa wanafunzi na wagonjwa na wakulima wasinge weza kusafurisha mazao yao, kupitia fedha hizi tumetengenieza barabara kwa Manispaa ya Bukoba eneo la kyebitembe tumeweka daraja na kufungua barabara inaunganisha kata Rwamishenye na Nshambya.

Ameongeza kuwa, “maana kuna mto kanoni wakati wa mvua wanafunzi wasingeweza kuvuka maana kulikuwepo kadaraja kadogo kwa sasa eneo hilo ni salama kwa wanafunzi pamoja na wananchi na barabara nyingine ni kimeya wilaya Muleba inaunganisha kata mbili kutoka kyamyorwa hadi kimeya mwanzoni haikuwepo walikuwa wanatembea umbali wa kilomita 21 kuitafuta Barabara kuu kwa sasa tumewatengenezea barabara ya kilomita tisa.”

Hata hivyo Mhandisi Avith amebainisha kuwa Serikali imeongeza ufanisi mkubwa ikiwemo kupata magari mapya na kutumia furusa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwani awali TARURA walikuwa wakitengewa bajeti ya shilingi bilioni 9.3 kwa mwaka lakini kwa sasa bajeti yao imepanda na kufikia kiasi cha bilioni 28.

Ally Kamwe: Tutaipiga Al Ahly Ligi ya Mabingwa
Thamani ya Madini: Wawekezaji wajenge Viwanda - Serikali