Abel Paul, Jeshi la Polisi – Arusha.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Nchini limesema zipo sheria zinazotoa miongozo na taratibu za matumizi sahihi ya Barabara hapa nchini huku likiwataka madereva kutokuwa chanzo cha huzuni kwa watanzania kwa kusababisha ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha ya Watanzania.

Hayo yamesemwa hii leo Desemba 23,2023 na Afisa mnadhimu namba moja wa kikosi cha Usalama Barabani Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Pili Misungwi katika kituo cha mabasi Jijini Arusha ana kubainisha kuwa wanaendelea na operesheni za ukaguzi na kutoa elimu nchi nzimaili kutomeza ajali.

Amesema, hivi karibuni kikosi hicho kilifanya uhakiki wa leseni nchi nzima ili kubaini madereva wenye sifa ambao wanapaswa kuendesha vyombo vya moto huku akibainisha kuwa kwa sasa wanahakiki madereva hao kama wanasifa za kuendesha vyombo husika hapa nchini.

Nao baadhi ya abiria wamesema operesheni hiyo imekuja wakati sahihi huku wakilipongeza Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kwa kuendelea kutoa elimu na kufanya operesheni hizo ambazo zimesaidia kupunguza ajali nchini.

Kwa upande wake Amini Khamis, Dereva wa basi la kampuni ya Hajis amesema wanaendelea kufuata sheria za usalama barabarani huku akibainisha kuwa elimu waliyopewa wataifanyia kazi.

Kitambi aahidi makubwa Geita Gold
Wanaume wanyooshewa vidole vipimo vya Kaswende