Kocha Mkuu wa Geita Gold, Denis Kitambi ameweka wazi kuwa atafanya mambo makubwa akiwa na kikosi hicho ikiwa ni baada ya kukisimamia kwenye mchezo wake wa kwanza.

Jumatano (Desemba 20) Kitambi ambaye alichukua mikoba ya Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuinoa Geita, alianza maisha yake ya kuinoa timu hiyo kwa kuiongoza kwenye mechi dhidi ya Singida Fountain Gate ambapo walishinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Kitambi amesema kuwa: “Mchezo wangu wa kwanza nikiwa ndani ya Geita Gold, wachezaji wamenionyesha namna ambavyo wanaweza kucheza kwa kujituma na kwa kufuata maelekezo yangu kama kocha mkuu.

“Kwa kiwango walichoonyesha katika mchezo uliopita dhahiri nimepata matumaini makubwa kuwa tunaweza kufanya mambo makubwa zaidi.

“Kikubwa ni kujituma wakati wowote tukiwa uwanjani, kwa bahati nzuri tunakwenda mapumziko kwa hiyo tutapata wasaa wa kuangalia palipopungua ili tupajazilizie, tukirudi tuwe kamilifu maeneo yote.”

Galtier akwepa kifungo Ufaransa
Madereva msiwe chanzo huzuni kwa Watanzania - ACP, Misungwi