Kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain, Christophe Galtier amefutiwa mashtaka ya ubaguzi wa rangi dhidi yake, aliyotuhumiwa wakati anakinoa kikosi cha klabu ya Nice inayoshiriki Ligue 1.

Galtier aliwekwa chini ya ulinzi na polisi mwezi Juni wakati anainoa PSG kabla ya kufukuzwa kazi baada ya tuhuma za ubaguzi wa rangi.

Madai hayo yalitokana na barua pepe iliyotumwa na mkurugenzi wa soka wa klabu ya Nice, Julien Fournier ambaye alimwandikia Sir Dave Brailsford mkuruenzi wa michezo wa INEOS inayomilikiwa na Sir Jim Ratcliffe, ambapo barua hiyo ilielezea mazungumzo yake na Galtier.

Inadaiwa, Galtier nwenye umri wa miaka 57 alizungumzia kuhusu matabaka ya wachezaji wa kikosi cha Nice ikihusisha imani za kidini pia.

Wachezaji kadhaa wa zamani wa Galtier walitoa ushahidi wakati wa kesi hiyo iliyodumu kwa juma moja ambayo ingemfanya bosi huyo wa zamani wa PSG, kutumikia kifungo cha miezi 12 jela na faini ya Euro 45,000 endapo angepatikana na hatia.

Hata hivyo, kesi ya Galtier imefutwa na mahakama baada ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya kocha huyo wa zamani na Fournier.

Mahakama pia ilisikiliza ushahidi kutoka kwa wachezaji kadhaa wa zamani wa Galtier ambao walidai kuwa waliathirika kiakili kutokana na vitendo vya ubaguzi wa rangi.

Beki wa Nice, Jean Clair Todibo alidai kwamba alizuiwa kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Galtier, hivyo hivyo kipa wa zamani wa klabu hiyo Teddy Boulhendi na kiungo wa kati Hlicham Boudaoui, miongoni waliokatazwa kufunga mwezi wa Ramadhani.

TPLB yafumua ratiba Ligi Kuu
Kitambi aahidi makubwa Geita Gold