Wazee Jamii ya kimasai wanaoishi katika Kijiji cha Itipingi Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya, wametakiwa kukemea mila potofu ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji, katika Jamii.

Rai hiyo imetolewa na Polisi Kata ya Mawindi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Daniel Joseph alipotembelea Kijiji hicho kilichopo ndani ya Kata yake.

Amesema, Wazee hao wanatakiwa kukemea mila potofu ndani Jamii ili kupunguza vitendo vya kihalifu kama vile ukeketaji, ubakaji, ulawiti pamoja imani za kishirikina ikiwemo upigaji wa ramri chonganishi.

Aidha, amewataka pia kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, ili Jeshi la Polisi liweze kufanyia kazi taarifa hizo ikiwemo kuwakamata wale wote wanaohusika na uhalifu wa namna yoyote ile na kuwafikisha mahakamani.

Wananchi wakumbushwa tahadhari Mvua za El-nino
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 24, 2023