Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amewataka Wananchi kuendelea kuchua tahadhari ya Mvua za El-nino kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini, TMA.
Kanali Abbas ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, ikiwa ni sehemu ya kuwatakia heri ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya wa 2024 Wananchi wa Mtwara.
Amesema, “tumechukua tahadhari maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu, lakini ni lazima tuwatahadharishe wananchi kuchukua hatua zaidi ikiwemo wale wanaoishi maeneo yanayojaa maji kuondoka na kuhamia maeneo ya miinuko.”
Kuhusu hali ya Usalama, Kanali Abbas amesema hali ni shwari na Wananchi waendelee kutii sheria za nchi bila shuruti wakati wote wa sikukuu za Krismass na Mwaka mpya.