Lydia Mollel – Morogoro.

Harakati za Kudhibiti na kupambana na utumiaji  dawa za kulevya kwa mkoa wa Morogoro bado zinaendelea, huku idadi kubwa ya wanaojitokeza kupata matibabu kwa asilimia 90 ni wakiwa ni Wanaume

Akizungumza katika ziara iliyoandaliwa na mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya – DCEA, iliyofanyika katika kliniki ya Waraibu wa dawa za kulevya kihonda, Dkt. Sosteusi Jeff Hongo amesema hata hivyo mwitikio wa waraibu waliojitokeza kwenye kliniki tangu ilipoanzishwa  ni mkubwa.

Naye mmoja wa watu waliowai kuwa waraibu wa dawa za kulevya, Verian Kunambi amesema kwa miaka kumi iliyopita na kwa sasa anawasaidia waraibu wengine kupata elimu na tiba ya methadone, huku akiwataka waraibu wanaopata matibabu kuendelea kuhudhuria kliniki bila kuchoka, kwani kuachana na madawa ya kulevya inawezekana.

Aidha Mkuu wa Gereza la kihonda ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Kliniki hiyo, SP. Lucas Mboje amewaomba Waandishi wa Habari kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuepukana na utumiaji wa dawa za kulevya, kwani madhara ya dawa hizo sio kiafya tu bali inaharibu hadi malengo ya mtumiaji.

Baadhi ya waraibu wanaondelea kuapata huduma katika kituo hicho, nao wamesema tangu wapate huduma wanaendelea vizur na wanategemea kupona kabisa na kurejesha utimamu wao wa akili walioupoteza hapo awali.

Hata hivyo, jamii mekumbushwa kufahamu kuwa mraibu wa dawa za kulevya ni mgonjwa kama wagonjwa wengine, hivyo wasiwatenge na kuwanyanyapaa bali kwa pamoja wawasaidie kupata elimu na tiba, katika vituo vya afya vilivyo karibu nao.

 

Kagera wajipanga mapokezi ya Chuo Kikuu Nelson Mandela
Anayetumia Baiskeli kutoa elimu azawadiwa Pikipiki