Viongozi katika jimbo la Plateau wamesema idadi ya watu waliopoteza maisha katika mfululizo wa mashambulizi ya Vikundi vya watu wenye silaha katika vijiji kadhaa katikati mwa Nchi ya Nigeria imefikia 160 huku zaidi ya 300 wakijeruhiwa.

Watu hao wenye silaha walivamia vijiji visivyopungua 20 Wilayani Bokkos na  kuwashambulia raia kisha kuwauwa watu 113 na kuzichoma moto nyumba kadhaa.

Monday Kasah, ambaye ni Kiongozi wa Serikali ya Wilaya ya Bokkos amesema majeruhi hao 300 walipelekwa kwenye Hospitali za Wilaya hiyo, wengine kwenye mji mkuu wa jimbo Jos na wengine Wilaya jirani ya Barkin Ladi.

Aidha, inaarifiwa kuwa katika Wilaya hiyo ya Barkin Ladi watu wengine wasiopungua 50 waliuwawa na magenge hayo ya wahuni, ikitaarifiwa kuwa chanzo cha matukio ya namna hiyo kikiwa ni imani za kidini na mizozo ya Wakulima na Wafugaji.

Malimwengu: Hoteli yenye Vitanda juu ya Mwamba
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 26, 2023