Jumla ya Watu 16 wameuawa kufuatia shambulio lililotokea kijiji cha Mushu kilichopo kaskazini kati jimbo la Plateau Nchini Nigeria, eneo ambalo hukumbwa na mapigano baina ya jamii za wakulima na wafugaji kila mara.

Kwa mujibu wa taarufa iliyotolewa na Jeshi nchini humo imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa manane kuamkia Desemba 24, 2023 ambapo milio ya risasi ilisikika na Washambuliaji waliwauwa na kuwajeruhi baadhi ya wanakijiji na wengine kutekwa.

Plateau ni jimbo linapatikana mpaka unaotenganisha eneo la kaskazini mwa Nigeria lenye idadi kubwa ya waislamu na kusini kukiws na wakristo wengi ambapo kwa miaka kadhaa limekuwa kitovu cha mivutano ya kikabila na kidini.

Inaarifiwa kuwa wengi wa jamii ya wafugaji ni waislamu na wakulima ni wakristo na mara kadhaa pande hizo mbili zimekuwa zikitumbukia kwenye mapigano ya kugombea ardhi na wakati mwingine mizozo ya imani za kidini.

Taarifa zisizojitosheleza: Jeshi lavionya Vyombo vya Habari
Taasisi za Dini zipambanie ufundi, ujasiriamali - Kinana