Watu wawili wamethibitishwa kufariki huku wengine ambao idadi yao haijajulikana mara moja wakijeruhiwa, baada ya basi Kampuni ya Mash Poa walilokuwa wakisafiria kupata ajali nchini Kenya.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema, basi hilo lilipinduka baada ya kugongana ana kwa ana na Lori lenye tela katika eneo la Taru usiku wa kuamkia leo Desemba 24, 2023.

Mkuu wa Polisi eneo la Samburu, Lydia Mambo amethibitisha ajali hiyo na kusema basi la Mash Poa  lilikuwa likitoka Nairobi kuelekea Mombasa na Lori hilo likuwa likielekea Nairobi kutoka Mombasa.

Amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi na kukosa umakini kwa madereva wote huku akidai majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Mariakani kwa matibabu zaidi na kuwataka madereva kuwa makini kuzingatia sheria za barabarani.

Anayetumia Baiskeli kutoa elimu azawadiwa Pikipiki
Uchaguzi DRC: Wagombea wa upinzani kuandamana